Friday, April 13, 2012

UAE YAFUTA MCHEZO WAKE WA KIRAFIKI NA IRAN.

SERIKALI ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE, limefuta mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Iran uliokuwa uchezwe April 17 mwaka huu. Sababu kubwa za kufutwa kwa mchezo huo inaelezewa kuwa ni suala la kisiasa baada ya jana Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad kutembelea kisiwa cha Abu Masa ambacho kipo kusini mwa mkoa wa Hormozgan. UAE inadai kuwa kisiwa hicho ni himaya yao na kwa tukio hilo la Ahmadinejad serikali ya nchi hiyo imeamua kumuita balozi wao aliopo nchini Iran pamoja na kusitisha mchezo baina ya nchi hizo mbili ambazo ni majirani. Katika taarifa iliyotolewa na gazeti moja nchini Iran imesema kuwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo limepanga kukutana na Shirikisho la Soka la UAE ili kuangalia uwezekano wa kuendelea na ratiba ya mchezo huo kama kawaida. Wakati ikiwa hakuna mkataba rasmi uliofikiwa baina ya mashirikisho ya soka ya nchi zote mbili kuhusiana na mchezo huo wa kirafiki, muingiliano wa kisiasa katika michezo unaweza kuleta utata kwa Shirikisho la Soka la bara la Asia au Shirikisho la soka la Dunia-FIFA na kupelekea kuingilia suala hilo.

No comments:

Post a Comment