Thursday, June 28, 2012
WAARABU KUMLIPA GYAN PAUNDI 140,000 KWA WIKI.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Sunderland, Asamoah Gyan anatarajiwa kusaini mkataba wa kudumu wa miaka mitano na klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu-UAE ambako alikuwa akicheza kwa mkopo ambapo atakua akilipwa paundi 140,000 kwa wiki na klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti moja la michezo nchini Ghana klabu ya Sunderland itavuna kiasi cha paundi milioni 21 kutoka kwa Al Ain kwa kumnyakuwa mshambuliaji huyo moja kwa moja ambaye mkataba wake wa mkopo ulikuwa unamalizika msimu huu. Mkataba huo mnono utakuwa umeipa faida kubwa Sunderland ambao walinyakuwa mshambuliaji kutoka klabu ya Rennes ya Ufaransa kwa ada ya paundi milioni 13 baada ya kung’aa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ghana. Baada ya kutua Sunderland aliwashtusha wadau soka pale alipokubali klabu hiyo kumtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Al Ain kwa ada ya paundi milioni 6 Septemba mwaka 2011 ambapo akiwa huko alifanikiwa kushinda mabao 27 katika michezo 24 liyocheza na kuiwezesha klabu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu ya huko ambayo inafahamika kama Pro League.
No comments:
Post a Comment