Wednesday, June 6, 2012

CARBALLO KUCHEZESHA PAMBANO LA UFUNGUZI EURO 2012.

Carlos Velasco Carballo.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limemtaja mwamuzi Carlos Velasco Carballo kutoka Hispania kuwa ndiye atakayechezesha mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Ulaya katika ya Poland ambao ni wenyeji wa michuano hiyo na Ugiriki katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Warsaw nchini humo. Carballo ambaye ana umri wa miaka 41 alikuwa ni mmoja wa waamuzi waliokuwepo wakati wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa mwezi uliopita baina ya Chelsea na Bayern Munich. Mwamuzi huyo ambaye alianza kuchezesha mechi za kimataifa mwaka 2008 pia alichezesha pambano la fainali ya Kombe la Ligi ya Ulaya au Europa League mwaka 2011 ambalo Porto waliibuka mabingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga Braga bao 1-0. Michuano hiyo ya Ulaya ambayo inatarajiwa kuanza Ijumaa Juni 8 itamalizika Julai 1 kwa mchezo wa fainali utakaochezwa jijini Kiev, Ukraine.

No comments:

Post a Comment