Friday, May 18, 2012

VILLA YAFANYA MAZUNGUMZO NA SOLSKJAER KUZIBA NAFASI YA MACLEISH.

Ole Gunnar Solskjaer
Klabu ya Molde ambayo inanolewa na nyota wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer imesema kuwa kocha huyo yuko katika mazungumzo na klabu ya Aston Villa kuangalia uwezekano wa kuwa kocha mpya wa timu hiyo. Villa kwasasa inatafuta mbadala wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Alex McLeish ambaye alitimuliwa kuinoa klabu hiyo baada ya miezi 11 kupita. Katika taarifa zilizosambaa nchini Uingereza zilieleza kuwa Solskjaer alionekana katika ndege binafsi ya mmiliki wa Villa, Randy Lerner wakielekea Birmingham kwa ajili ya mazungumzo. Solskjaer ambaye ana miaka 39 amekuwa akiifundisha Molde toka Novemba mwaka 2010 na kuingoza timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Norway katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment