Wednesday, May 23, 2012

VILLA KUIKOSA EURO 2012.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Hispania, David Villa anatarajiwa kukosa kuiwakilisha nchi yake katika michuano ya Ulaya mwaka huu kutokana na majeruhi yanayomsumbua baada ya kuvunjika mguu. Villa ambaye ana umri wa miaka 30 alimwambia kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Vicente del Bosque kuwa hatakuwa katika hali nzuri kipindi cha mashindano hayo kutokana na majeraha hayo ya kuvunjika aliyopata Novemba mwaka jana. Mchezaji huyo aliandika katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa twitter akiwaomba msamaha mashabiki wake uamuzi wake huo pamoja na wachezaji wenzake wa timu ya taifa. Villa ndiye anashikilia rekodi ya mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika timu ya Hispania akiwa amefunga mabao 51 katika michezo 82 aliyocheza. Hispania ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo wako katika kundi C pamoja na timu za Italia, Jamhuri ya Ireland na Croatia pia watamkosa beki wake mkongwe Carles Puyol ambaye nae anauguza majeraha ya mguu.

No comments:

Post a Comment