Monday, May 21, 2012

TORRES MGUU NJE MGUU NDANI.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Chelsea Fernando Torres anatarajia kufanya mazungumzo na klabu yake hiyo kuhusiana na mustakabali wake baada ya kuikosoa klabu hiyo kwa mambo ambayo wamemfanyia. Torres ambaye ni raia wa Ufaransa amekiri kuwa ni jambo ambalo hakulitegemea katika maisha yake ya soka kuanza katika benchi la wachezaji wa akiba wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambapo timu yake hiyo iliiibuka kidedea. Mshambuliaji huyo ambaye alihamishwa kwa ada ya pauni milioni 50 kutoka klabu ya Liverpool Januari mwaka jana ameifungia Chelsea mabao sita katika Ligi Kuu nchini Uingereza na kufikisha mabao 11 katika mashindano yote aliyocheza msimu huu. Akihojiwa na gazeti moja la nchini kwao Torres amesema kuwa msimu huu haukuwa mzuri kwake lakini klabu hiyo imekuwa ikimfanyia mambo ambayo hakuyategemea kwani katika kipindi hiki cha mwishoni mwa msimu anadhani kiwango kilikuwa kizuri na alistahili kuanza katika kikosi cha kwanza. Alimalizia kuwa alijisikia vibaya wakati alipoangalia orodha ya kikosi ambacho kilicheza mchezo huo na kuona jina lake halikuwepo kwani alidhani angeanza kucheza mchezo huo.

No comments:

Post a Comment