MWAMUZI aliyechezesha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu nchini Uingereza baina ya timu ya Manchester City na Queens Park Ranger-QPR, Mike Dean amekiri kuwa kama angeona tukio la mkwaruzano baina ya Carlos Tevez na Joey Barton wa QPR asingesita kumpa kadi nyekundu Tevez katika mchezo huo. Barton alionyeshwa kadi nyekundu na Dean katika mchezo huo baada ya kumpiga kiwiko Tevez na baadae tukio lake la kuwafanyia vurugu wachezaji wengine wa City Sergio Aguero na Vincent Kompany na kupelekea kuongezewa adhabu na kufungiwa mechi 12. Lakini Dean amekiri kupitia picha ya video aliyoiona kuwa Tevez ambaye hakupewa adhabu katika mchezo huo na alistahili kuadhibiwa kutokana na tukio lake la kumkwatua makusudi Barton. Mwamuzi huyo aliendelea kusema kuwa ni bahati mbaya tukio lile hakuliona na wasaidizi wake wa pembeni nao pia hawakuliona. Mbali na Barton kufungiwa mechi 12 lakini pia mchezaji huyo ametozwa kiasi cha paundi 75,000 ambapo klabu yake imesema inachunguza tukio hilo kwa makini kabla ya kukata rufani.
Saturday, May 26, 2012
TEVEZ ALISTAHILI KADI NYEKUNDU - DEAN.

No comments:
Post a Comment