Friday, May 18, 2012

TENGA AMMWAGIA SIFA KIM POULSEN.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini-TFF Leodgar Tenga amemmwagia sifa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen ambaye amechukua nafasi ya raia mwenzake kutoka Denmark Jan Poulsen. Tenga pia amesema kuwa TFF inaamini kuwa Poulsen ndio mtu sahihi wa kuleta mabadiliko katika kikosi cha timu ya taifa-Taifa Stars ili kurejesha makali yake kama zamani. Kocha huyo ambaye ana umri wa miaka 32 alikuwa akiifundisha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 na 20 ambapo mara baada ya kuchukua mikoba hiyo aliwaondoa wachezaji wenye umri mkubwa waliokuwepo katika timu hiyo. Tenga amesema kuwa wana matarajio makubwa na kocha huyo mpya ambaye ameonyesha uwezo wa wachezaji chipukizi ili waweze kuisaidia timu hiyo katika kwa siku za baadae. Mara baada ya uteuzi wake huo Poulsen aliteua kikosi cha timu ya taifa ambacho kimekuwa hakina wakongwe waliozoeleka kama Nadir Haroub, Henry Joseph, Nizal Khalfan na Abdi Kassim.

No comments:

Post a Comment