Thursday, May 24, 2012

SIJAFIKIRIA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA - GERRARD.

KIUNGO wa kimataifa wa timu ya taifa Uingereza, Steven Gerrard ametupilia mbali suala la kustaafu soka la kimataifa mara baada ya michuano ya Kombe la Ulaya mwaka huu. Mchezaji huyo mwenye miaka 31 ambaye atakiongoza kikosi cha nchi hiyo karika michuano ya hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Poland na Ukraine amesema kuwa anataka kumuonyesha kocha mpya Roy Hodgson kuwa anaweza kuendelea kuitumikia timu hiyo mpaka kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2014 litakalofanyika nchini Brazil. Akihojiwa Gerrard amesema anatambua kuwa katika umi aliofikia watu wataanza kuweka maswali na kumuuliza kama anatakiwa kustaafu kuichezea Uingereza na kuelekeza nguvu zake katika klabu ya Liverpool lakini yeye hafikirii suala hilo. Hata hivyo kiungo huo amekiri kuwa ni lazima kwanza aonyeshe kiwango bora katika michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza June 8 na kumalizika Julai 1 mwaka huu ili kumvutia kocha huyo.

No comments:

Post a Comment