Tuesday, May 1, 2012

ROCK STAR GALLAGHER AVAMIA POST-MATCH PRESS CONFERENCE BAADA YA KUPAGAWA NA USHINDI WA CITY.

Gallagher akiwa na Maradona mara baada ya mchezo wa Manchester City na  Manchester United.
MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa rock nchini Uingereza, Liam Gallagher ambaye ni mshabiki wa timu ya Manchester City amevamia mkutano wa waandishi wa habari na timu hiyo baada ya kikosi hicho kinachonolewa na Roberto Mancini kuwafunga wapizani wao Manchester United. Beki wa City Vincent Kompany ndiye alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi kwa kichwa na kuipeleka timu yake kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa bendi maarufu nchini humo ya Oasis alivamia chumba cha mkutano na kukaa katika kiti cha Mancini ambaye alikuwa bado hajaingia mkutanoni pembeni ya Kompany. Gallagher aliwaambia wana habari waliopo hapo kuwa ana mpenda kocha mkuu wa klabu hiyo Mancini huku akimponda Ferguson kwamba kwa muda ule lazima atakuwa amekwenda kunywa pombe ili kupunguza machungu ya kufungwa. Mara baada ya kusema hayo mwanamuziki huyo aliondoka eneo hilo huku akimkumbatia na kumpongeza Kompany ambapo baadae alikutana na nguli wa soka wa zamani kutoka Argentina Diego Maradona ambaye alikuja kumtizama mkwewe ambaye ni mshambuliaji wa City Sergio Aguero.

No comments:

Post a Comment