Wednesday, May 16, 2012

OBAMA AMTANIA BECKHAM KATIKA HAFLA WHITE HOUSE.

RAIS Marekani Barack Obama amemtania mchezaji nyota mkongwe wa kimataifa wa Uingereza David Beckham wakati wa sherehe za kuipongeza timu ya Los Angeles Galaxy iliyonyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo katika Ikulu ya nchi hiyo. Mbali ya kumtania mchezaji huyo Obama pia alimsifu mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid kwa ujasiri wake wakupambana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita huku akisaidia timu hiyo kunyakuwa ubingwa huo. Rais huyo wa taifa linaloogopeka ulimwenguni alimtania Beckham mwenye umri wa miaka 37 kutokana na kuonekana katika mabango ya matangazo nchini humo akitangaza nguo za ndani. Mara baada ya hotuba iyo fupi ya kuibaribisha timu hiyo Beckham alijiungana na wahezaji wenzake London Donovan ambaye pia anaihezea timu ya taifa ya Marekani na nyota wa zamani wa Jamhuri ya Ireland Robbie Keane katika sherehe zilizoandaliwa katika ukumbi wa mashariki kwenye ikulu ya nchi hiyo. Beckham ambaye ameichezea timu ya taifa ya Uingereza michezo 115 anataka kurejea tena katika anga za kimataifa mwaka huu kukiongoza kikosi cha nchi yake kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London baadae mwaka huu.

No comments:

Post a Comment