Tuesday, May 15, 2012
NEYMAR, GANSO KUIKOSA DENMARK.
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar na kiungo wa timu hiyo Paulo Henrique Ganso watakosa mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Denmark baada ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo-CBF kukubali kuwaachia wachezaji hao waitumikie klabu yao ya Santos. Katika taarifa yake CBF imesema kuwa wakubali ombi la Santos kuwaachia wachezaji hao kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la klabu Bingwa ya Amerika Kusini dhidi ya Velez Sarsfied ya Argentina mchezo ambao utachezwa Mei 24 mwaka huu ikiwa ni siku mbili kabla ya Brazil haijakutana na Denmark jijini Hamburg. Ganso anaonekana ndio atakuwa kiungo tegemeo katika kikosi cha Brazil kitachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 wakati Neymar mwenye miaka 20 yeye ndiye mshambuliaji nyota pekee ambayo nchi hiyo imetoa katika miaka michache iliyopita. Brazil pia inatarajiwa kucheza na Mexico jijini Dallas, Marekani June 3 mwaka huu kabla ya kukwaana na Argentina jijini New Jersey siku sita baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment