Sunday, May 13, 2012

MISS TANZANIA-BY JANETH JACKSON -UHONDO FROM LAST WEEK

mbeleni.nafahamu kuwa endapo utaingia matatizoni basi ni sote tutakuwa tuko katika matatizo.Tatizo

langu ni lako na lako langu ndio maana tunahitaji sana kushauriana kwa kina kabla ya kufanya

jambo.”

“Andrew najua una wasiwasi mwingi kuhusu mimi na Vero.Hilo ni kubwa linalokuumiza kichwa.Hata mimi

sijisikii vizuri kumtesa Vero binti aliyeyatoa maisha yake kwangu.Binti anayenipenda kwa dhati ya

moyo wake.Ni vero huyu huyu ndiye aliyeirudisha tena furaha ndani ya moyo wangu na kuliondoa wingu

zito la ukiwa lililokuwa limenifunika.Nampenda Vero lakini sina jinsi ni lazima nionane na Happy.”

Andrew aliinuka kitini akaiendea friji na kujimiminia mvinyo baridi akanywa mafunda kadhaa kisha

akamgeukia Patrick.

“Ok Patrick kwa sababu umekwishaamua basi hatuna budi kufanya hivyo.Mimi nitaianza kazi hiyo

kesho.Nitamtafuta mtu ambaye ataifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa.Usijali kuhusu hili rafiki
yangu”

Patrick alifurahi akainuka na kumkumbatia rafiki yake.
********************************************************************

Saa kumi na mbili za jioni Veronika alirejea katika shughuli zake na kumuaga mama yake kuwa

alikuwa akaienda kumwangalia Patrick anaendelaje.Ni siku ya tatu sasa toka Patrick atoke

hospitali.Hali yake haikuwa ikiendelea vizuri sana.Muda mwingi alikuwa akionekana ni mtumwenye

mawazo mengi sana.Hali hii ilimpa wasiwasi mwingi Vero kiasi cha kumfanya awe karibu naye kila

wakati ili kujaribu kumchangamshana kumrudisha katika hali yake ya kawaida.

Ingawa Patrick alijitahidi kwa kila jinsi ili Vero asione hali hii ya unyonge lakini mara nyingi

alishindwa na kujikuta akitoa machozi.Vero aliigundua hali hii nakwa kiasi kikubwa ikamuongezea

udadisi juu ya kinachoendelea.alijua ni lazima liko jambo ambalo linamchanganya Patrick .

‘Haloo sweetie”Alisema Vero baadaya kuingia ndani kwa Patrick

“Haloo vero, you are back”akasema Patrick

Vero akamfuata Patrick kitandani akamkumbatia na kumpiga busu zito.

‘Unaendeleaje mpenzi”

“Naendelea vizuriMungu ananisaidia sana.Muda si mrefu nitapona kabisa”

Baada ya kujuliana hali Vero alimwandalia Patrick Juice kisha yeye akaelekea jikoni kufanya

maandalizi ya chakula cha jioni.Patrick alipata faraja kubwa baada ya Vero kuwasili Ni wazi

Patrick husikia furaha kubwa moyoni awapo na Vero.

Ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa bado alimpenda sana Vero lakini kwa ghafla Happy ametokea na

kuanza taratibu kuzihamisha hisia zake.

Chakula kiilpokuwa tayari kikawekwa mezani,wakala kisha wakapumzika na baadae wakaelekea kulala.

“Vero dear tayari umekwisha kata tiketi za kuingia Miss Tanzania Jumamosi?Patrick akauliza

“Tayari mpenzi Nimekwishaziandaa .Je utaweza kweli kwenda na hali hii?Naona kama hali yako inazidi

kudhoofia siku hadi siku”

“Usijali mpenzi wangu lazima nihudhurie hata iweje.Nina imani ndani ya siku mbili tatu zijazo hali

yangu itakuwa shwari”

Vero akanyamaza kimya akajaribu kuvuta kumbukumbu nyuma siku ile Patrick alipoanguka na kupoteza

fahamu alikuwa akitazama kipindi cha wagombea wa miss Tanzania.Hakutaka kukubaliana kuwa kuna

kitu chochote kinachoendelea baina ya Patrick na mashindano yale.Alijitahidi kuilazimisha akili

yake ikubaliane na taarifa ya daktari kuwa Patrick alipoteza fahamu kwa sababu ya uchovu mwingi
uliokuwa ukimkabili kiasi cha kuufanya .



...daktari lakini kuna kitu kiko moyoni mwa Patrick ambacho
kinamyima raha na na kuisumbua akili yake namna hii.Ni kwa sababuhiyo tu ndiyo maana amepoteza

furaha yote aliyokuwa nayo kabla.Chakula chenyewe mpaka abembelezwe.mara kadhaa nimemfuma mwenyewe

kwa macho yangu akilia.Ingawa anajitahidi sana kuificha hali hii lakini nimekwishafahamu .Anyway

nitajitahidi kumuuliza ili anieleze kama kuna jambo lolote linalomsibu.”

Veronika alizama ghafla katika mawazo.

“Unawaza nini mpenzi wangu”Patrick akauliza

“Nothing.Siwazi chochote zaidi yako.Unajua Patrick hali yako kwa sasa inanipa wasiwasi sana.Tangu

umetoka hospitali umebadilika.Ni kitu gani kinakusumbua mpenzi hebu niambie.Hali hii inanifanya

hata mimi nihisi kama vile ninaumwa pia.Au kama kuna kitu nimekukosea niambie Patrick ili

nijirekebishe.Tangu tumeanza mapenzi yetu sijawahi hata siku moja kukuona katika hali hii”

Vero akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa kwikwi.
Patrick akamvutia Vero kwae akambusu na kumwambia

“Usihofu kitu baby hakuna kitu kingine kinachonisumbua .Kama daktari alivyosema kuwa natakiwa

kupumzika sana .Uchovu ndio uliopelekea tatizo lile kutokea.”

Alisema Patrick huku akizichezea nywele laini za Vero.

‘Hapana dear najua lazima kuna kitu kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia”

“Wow my dear angel ,wewe ndiye maisha yangu.Wewe ndiye uliyeyashika maisha yangu.Nimekukabidhi

funguo za moyo wangu.Wewe ndie mfariji wangu,wewe ndiye furaha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu

sasa kwa nini nikufiche kitu?Hakuna kitu nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu nahaitakuja tokea

nikawa na tatizo nikashindwa kukwambia.Sasa nisipokwambia wewe nitamwambia nani tena?”

Patrick alijitahidi kumtoa Vero wasiwasi aliokuwa ameanza kuwanao juu yake na mara moja akaazimia

moyoni kubadilika kitabia ili Vero asije akaendelea kumdadisi.Taratibu akaanza kurudikatika hali

yake ya kawida ya ucheshi na uchangamfu mkubwa kitu ambacho Vero alikifurahia

sana.
*****************************************************************

Ni juamamosi angavu ndaniya jiji laDar es salaam,jiji lililjaa kila aina ya pilika na

purukushani.Jua lilikuwa likielekea magharibi na kulipisha giza lichukue nafasi yake.Jioni hii

iliwakuta Patrick na Veronika wakiwa katika pilika pilika za kujiandaa kuelekea katika

kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa katika ukumbi wa Diamong jubilee.

Patrick ndiye aliyekuwa katika pilika pilika nyingi zaidi jioni hiyo.Siku hii ilikuwa ni moja kati

ya siku zake kubwa kabisa katika maisha yake.Ni siku ambayo aliamini ingemkutanisha tena na

kiumbe ampendaye kwa dhati ya moyo wake.Alikuwa ndani ya suti nzuri ya gharama kubwa.Suti hii huwa

anaivaa kwa nyakati maalum kamahizi.Hakika alikuwa amependeza vilivyo kijana huyu.Wakiwa katika

harakati z a kumalizia kujiandaa simu yake ikaita.Alkuwa ni Andrew.

“Haloo Andrew”

“Hallo Patrick vipi mko tayari?aliuliza Andrew huku akicheka kichinichini.

“Tupo tayari Andrew na muda wowote toka sasa tunaweza kuanza safari ya kuelekea ukumbini”

“Ok Patrick sisi tayari tumekwishajiandaa na muda wowote tutakuwa njiani kuelekea huko na

tutawasubiri nje ya ukumbi ili tuingie pamoja.Ila ndugu yangu nakuomba kitu kimoja katu

usihamaki.Wala usionyeshe aina yoyote ya mstuko pindi utakapomuona Happy.Najua tu lazima kunaweza

kutokea na kitu kama mstuko flani hivi ila tafadhali naomba ujaribu kujizuia kwa sababu pale
tutakuwa ..

ITAENDELEA ...USIKOSE JMAPILI  IJAYO





No comments:

Post a Comment