MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amefanikiwa kushinda kiatu cha dhahabu barani Ulaya baada ya kuongoza katika orodha ya wafungaji katika bara hilo. Messi amefanikiwa kufunga mabao 50 katika Ligi Kuu nchini Hispania na kumaliza msimu akiwa na mabao manne zaidi ya mpinzani wake Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akimkaribia. Messi alishindwa kupata bao Jumamosi wakati timu yake ilipotoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Real Betis katika mchezo wa mwisho kwa kocha Pep Guardiola kuinoa timu hiyo lakini alishindwa kufikiwa na Ronaldo ambaye alifunga bao moja wakati wa ushindi wa mabao 4-1 timu yake ya Real Madrid iliyopata dhidi ya Malaga. Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie yeye amemaliza msimu akiwa na mabao 30 lakini alishindwa kufunga wakati timu yake ilipofanikiwa kuifunga West Brom na kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya huku Wayne Rooney wa Manchester United akimfuatia kwa karibu baada ya kufunga mabao 27 msimu huu. Nafasi ya tano katika orodha hiyo inashikiliwa na Zlatan Ibrahimovic ambaye anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda kiatu cha dhahabu akiwa na vilabu viwili tofauti baada ya kufanikiwa kumaliza msimu akiwa na mabao 28 aliyoifungia klabu yake ya AC Milan.
Rank | Player | Country | Club | League | Weight | Goals | Points |
1 | | ARG | | ESP | 2 | 50 | 100 |
2 | | POR | | ESP | 2 | 46 | 92 |
3 | | NED | | ENG | 2 | 30 | 60 |
4 | | NED | | GER | 2 | 29 | 58 |
5 | | SWE | | ITA | 2 | 28 | 56 |
6 | | ENG | | ENG | 2 | 27 | 52 |
7 | | GER | | GER | 2 | 26 | 52 |
8 | | TUR | | TUR | 1.5 | 32 | 48 |
= | | NED | | NED | 1.5 | 32 | 48 |
= | | COL | | ESP | 2 | 24 | 48 |
= | | ARG | | ITA | 2 | 24 | 48 |
* = league season finished
No comments:
Post a Comment