Thursday, May 17, 2012
MAN UNITED YAMPIGA CHINI OWEN.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Uingereza, Michael Owen ameachwa na klabu yake ya Manchester United baada ya miaka mitatu isiyokuwa ya mafanikio aliyokaa klabuni hapo kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yaliyokuwa yakimsumbua. Owen alithibitisha kuachwa kwake katika mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuandika kuwa meneja wake Sir Alex Ferguson alimtaarifu kuwa klabu hiyo haiwezi kumuongeza mkataba mwingine tena. Mchezaji huyo aliwashukuru wachezaji, wafanyakazi na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wao katika kipindi cha miaka mitatu ambayo amekuwa akiitumikia klabu hiyo ambapo kwasasa amesema kuwa atapumzika kidogo akifikiria suala la kufanya. Owen mwenye umri wa miaka 32 amewahi kucheza katika vilabu vya Liverpool, Real Madrid na Newcastle ambapo mchezo wake wa mwisho akiwa na kikosi cha United ilikuwa ni Novemba mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment