Friday, May 25, 2012
BLATTER CALLS FOR ALTERNATIVE TO PENALTIES.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amemuomba rais wa heshima wa klabu ya Bayern Munich, Franz Beckenbauer kuangalia namna ya kuepuka janga la changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa soka. Beckenbauer ni kiongozi wa Kamati Maalumu iliyoteuliwa na FIFA ambayo itakuwa na jukumu la kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za mchezo huo. Blatter ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wajumbe katika mkutano wa shirikisho hilo leo ikiwa siku chache zimepita baada ya Chelsea kuifunga Bayern Munich kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Blatter amesema kuwa mchezo wa soka unaweza kuwa janga wakati imu zinapokwenda katika mikwaju ya penati kwani inapofikia huko mchezo huo unapoteza uhalisia wake. Aliendelea kusema kuwa pengine kamati ya Beckenbauer inaweza kutafuta njia nyingine ya kuamua mshindi badala ya matuta, inaweza isiwe leo lakini labda katika siku zijazo. Beckenbauer ambaye alishinda michuano ya Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani kipindi cha nyuma hakupatikana haraka kuzungumzia suala hilo lakini alishawahi kusema kipindi cha nyuma kuwa anaona afadhali kuwepo changamoto ya mikwaju ya penati kuliko suala la bao la dhahabu au fedha sheria ambazo ziliwahi kutumika kipindi cha nyuma.
No comments:
Post a Comment