Thursday, May 3, 2012

AZAM KUMJARIBU ODHIAMBO.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Randers ya Sweden, George Odhiambo ametua jijini Dar es Salaam baada ya kukubali mwaliko wa timu ya Azam FC. Odhiambo ambaye aliondoka nchini Sweden April mwaka huu baada ya mkataba wake kusitishwa anatarajiwa kufanya mazoezi na klabu hiyo itakayokuwa ikijiwinda na mchezo wake wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar. Wakala wa mchezaji huyo anayeitwa Ed Stoner athibitisha taarifa hizo za mteja wake kuondoka jijini Nairobi jana kuja Dar es Salaam na atakuwa katika klabu hiyo akifanya mazoezi pamoja na kukutana na benchi la ufundi kwakuwa hivi sasa mchezaji huyo yuko huru. Odhiambo ambaye aliwahi kunyakuwa taji la mchezaji bora wa mwaka 2010 katika Ligi Kuu nchini Kenya ameamua kurejea kucheza Afrika ili kujaribu kurejesha makali yake baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza katika klabu aliyotoka kumfanya atemwe katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya-Harambee Stars. Pamoja na kuhusishwa kutaka kuhamia katika klabu ya Gor Mahia, wakala amesema kwamba hakuna klabu yoyote mpaka hivi sasa waliyozungumza nayo kuhusiana na kumsajili mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment