Sunday, April 15, 2012

ZAMALEK YASHTUSHWA NA ADHABU ALIYOPEWA RAZAK.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limemfungia kucheza michezo minne bekiwa kimataifa kutoka Benin, Razak Omotoyossi anayekipiga katika klabu kongwe nchini Misri ya Zamaleck, baada ya kuzozana na mwamuzi aliyechezesha mchezo baina ya timu hiyo na African Sports wiki iliyopita. Mkurugenzi wa Zamaleki Hamad Anwar alionyesha kusikitishwa kwake na hatua hiyo ya CAF na kusema kuwa adhabu hiyo ni kali sana kulinganisha na kosa lenyewe hivyo wanaangalia uwezekano wa kukata rufani ili adhabu hiyo iweze kupunguzwa. Mshambuliaji huyo aligombana na mwamuzi katika mchezo huo wa Klabu Bingwa ya Afrika na wote wawili Razak na mwamuzi huyo raia wa Senegal walionyesha kukasirika ingawa katika majibioshano yao hakuna aliyewaelewa kwasababu walikuwa wakizungumza lugha ya kifaransa. Omotoyossi alijiunga na Zamaleki Octoba mwaka jana ambapo sasa anatarajiwa kukosa michezo miwili inayofuata dhidi ya Maghreb de Fas ya Morocco. Toka atue katika klabu hiyo mchezaji huyo ameshafunga mabao manne likiwemo bao moja dhidi ya Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment