Tuesday, April 17, 2012

WILSHERE NJE EURO 2012.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wa klabu hiyo Jack Wilshere atakosa kushiriki michuano ya Ulaya kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu yanayomsumbua. Wilshere mwenye umi wa miaka 20 hajacheza mchezo wowote msimu huu na baada ya Arsenal kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu kwa kufungwa mabao 2-1, kocha akasema kuwa mchezaji hawezi kuwa amepona kabisa kwa ajili ya michuano ya Ulaya itakaypfanyika Poland na Ukraine Juni mwaka huu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema kuwa kiungo huyo hawezi kucheza tena msimu huu na pia michuano ya Ulaya kwa kuwa anapona maumivu ya kifundo cha mguu polepole. Mchezaji mpaka sasa ameshacheza michezo mitano tu timu ya taifa ya Uingereza toka alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment