Tuesday, April 3, 2012

PARK ATABIRI KOMBE LA DUNIA KWENDA ASIA NDANI MUONGO MMOJA.

KIUNGO wa Manchester United Park Ji-Sung ametabiri kuwa nchi moja kutoka bara ya Asia itanyakuwa Kombe la Dunia ndani ya miaka 10 ijayo. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Korea Kusini alinukuliwa na gazeti moja nchini China akisema kwamba timu za bara la Asia bado zina safari ndefu kufikia mafanikio hayo lakini watafikia huko haraka. Park amesema kuwa bado kuna nafasi kubwa kati ya Asia na timu za Ulaya ambazo ndio zinaongoza duniani kwa soka hivyo wana safari ndefu ingawa katika miaka ya karibuni wamekuwa wakionyesha soka safi ambalo wanaweza kulingana na timu za huko. Mpaka sasa kiwango bora kilichoonyeshwa na timu kutoka bara la Asia ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 2002 wakti Korea Kusini ilipokuwa mwenyeji wa michuano hiyo na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali. Michuano mingine ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil ikifuatiwa na itakayofanyika Russia 2018 na ile Qatar 2022.

No comments:

Post a Comment