Wednesday, April 4, 2012
NYOTA WA ZAMANI WA MADRID AFARIKI.
KLABU ya Real Madrid imesema kuwa nyota wake wa zamani Jose Maria Zarraga ambaye aliisaidia timu hiyo kushinda mara tano mfululizo michuano ya Kombe la Ulaya amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 81. Zarraga alikuwa akicheza nafasi ya kiungo katika kikosi ambacho walikuwepo nyota wengine kama Alfredo di Stefano na Ferenc Puskas kikosi ambacho kilishinda michuano ya Kombe la Ulaya mfululizo kuanzia mwaka 1956 mpaka 1960 pamoja na mataji sita ya Ligi Kuu nchini Hispania. Nguli huyo katika kipindi chake alifunga mabao 96 katika michezo 306 aliyoichezea klabu hiyo ambayo alijiunga nayo mwaka 1949 kabla ya kujumuishwa katika kikosi cha kwanza miaka miwili baadae, aliondoka Madrid mwaka 1962 akiwa na miaka 32. Taarifa kutoka klabuni hapo imesema wachezaji watasimama dakika moja kwa ajili ya kutoa heshima kwa Zarraga wakati wa mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa ya Ulaya baina ya timu hiyo na APOEL Nicosia katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
No comments:
Post a Comment