Wednesday, May 2, 2012

SIJASHANGAZWA NA UTEUZI WANGU - hODGSON.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema kuwa hakushangazwa na uteuzi wake wa kukalia kiti hicho ambacho kiliachwa na Fabio Capello pamoja na kwamba wengi walitabiri Harry Redknapp angechukua nafasi hiyo. Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA David Bernstein alifafanua kuwa kamati teule ambayo ilikuwa na watu wanne ambao walikuwa wanataka nafasi hiyo tayari ilikuwa imeshafanya maamuzi ya kumteua Hodgson ambaye alikuwa kocha wa West Brom mwezi mmoja uliopita. Hodgson ambaye ana umri wa miaka 64 alikabidhiwa mkataba wa miaka minne wa kuinoa timu hiyo jana ambapo alisisitiza kuwa rekodi yake nzuri na uzoefu alionao ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kupata kibarua hicho. Kocha huyo amekiri kuwa bado ana changamoto kubwa ya kujaribu kurejesha imani ya wachezaji kwake wakiwemo wale ambao walikuwa wakimpa nafasi kubwa Redknapp kuchukua nafasi hiyo baada ya Capello kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment