Saturday, May 19, 2012

SIDHANI KAMA ABRAMOVICH ATAMPA KAZI DI MATTEO - ZENDEN.

Bolo Zenden.
KIUNGO wa zamani wa Chelsea Bolo Zenden hategemei mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich atampa mkataba wa kudumu Roberto Di Matteo wa kuinoa timu hiyo hata akiweza kuifunga Bayern Munich katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya unaotarajiwa kufanyika leo. Zenden alisisitiza kuwa Di Matteo ameshafanya mengi mazuri toka alipochukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo baada ya Andre Villas-Boas alipotimuliwa lakini anaamini kuwa Abramovich atatafuta kocha mwingine kwa ajili ya kuonoa klabu hiyo msimu ujao. Nyota huyo wa zamani aliendelea kusema kuwa ni ngumu sana kwani kwa mawazo yake anadhani Di matteo angepewa kibarua hicho kwasababu ameisaidia kushinda Kombe la FA na pia alifanikiwa kurejesha makali ya timu hiyo wakati wakiwa katika hali mbaya. Wakati baadae ana nafasi pia ya kushinda michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya taji ambalo Abramovich alikuwa akilitaka siku nyingi lakini kwa jinsi Zenden anavyomfahamu bosi huyo atatafuta kocha mwingine ambaye ana uzoefu zaidi ya Di Matteo.

No comments:

Post a Comment