Monday, May 21, 2012

NAPOLI YAWAHARIBIA JUVE.

Marek Hamsik
TIMU ya Napoli ya nchini Italia imefanikiwa kuwafunga mabao 2-0 mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo, Juventus katika fainali ya Kombe la Italia iliyochezwa jana na kuifanya timu hiyo kunyakuwa taji lake la kwanza baada ya miaka 22. Hicho kinakuwa kipigo cha kwanza kwa klabu ya Juventus katika mashindano yote msimu huu wakiwa wameshinda michezo 26 na kutoa sare michezo 16. Mara ya mwisho kwa Napoli kunyakuwa taji ilikuwa ni mwaka 1990 wakati waliposhinda kombe la Ligi kuu ya nchi hiyo wakati mara ya mwisho kunyakuwa kombe la Italia ilikuwa ni mwaka 1987. Katika michezo mingine ya kufunga msimu wa ligi za nchi hiyo timu ya Torino ilifanikiwa kupanda kucheza ligi kuu msimu ujao baada ya kukosekana kwa miaka mitatu kwa kuwafunga Morena mabao 2-0 wakati Pescara nao wakiungana na Torino baada ya kuifunga Sampdoria mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment