Saturday, May 19, 2012

ADHABU YA ROONEY NI FAIFA KWETU - NASRI.


 

KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Manchester City, Samir Nasri amesema kuwa kufungiwa michezo miwili kwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza ni nafasi nzuri kwa nchi yake ambayo itakutana na nchi hiyo katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Ulaya mwaka huu. Ufaransa ambayo imekuwa ikitolewa katika hatua ya makundi katika michuano ya Ulaya mwaka 2008 na Kombe la Dunia 2012, watakutana na Uingereza June 11 jijini Donetsk kabla ya kucheza na wenyeji wenza Ukraine na baadae Sweden katika kundi lao. Nasri amesema kuwa Ufaransa ina uwezo wa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwakuwa na kikosi kizuri na chenye ushindani na kuongeza kuwa ni vizuri zaidi kucheza na Uingereza mchezo wa kwanza huku mshambuliaji wake tegemeo akiwa bado anatumikia adhabu yake. Rooney alifungiwa michezo miwili kufuatiwa kutolewa nje baada ya kumkwatua beki wa timu ya Montenegro, Miodrag Dzudovic wakati wa mchezo wa mwisho wa kufuzu michuano hiyo uliofanyika Octoba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment