Tuesday, April 3, 2012

UONGOZI WA AL WASL WAMKINGIA KIFUA MARADONA.

KLABU ya Al Wasl ya Dubai imesema kwamba kocha wao, Diego Maradona alifanya jambo la heshima baada ya kuteremika jukwaani kuwavaa mashabiki waliokuwa wanamzomea mpenzi wake na wake za wachezaji wa klabu hiyo. Al Wasl imesema kwenye tovuti ya klabu hiyo leo kwamba hasira za Maradona zilikuwa zinaeleweka na alifanya jambo la heshima mwishoni mwa wiki. Abdullah al-Bishr pia alimuomba radhi gwiji huyo wa Argentina, ambaye alianza kuifundisha timu hiyo mwaka jana. Maradona alipambana na mashabiki wa timu pinzani, Al Shabab ambao waliwazomea wanawake wa wachezaji wa timu yake ambayo katika mchezo huo walifungwa mabao 2-0. Maradona aliwaita mashabiki wa Al Shabab ni waoga.

No comments:

Post a Comment