Sunday, April 15, 2012

KIFO CHA MOROSINI CHAMLIZA BLATTER.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amekiri kuwa ameshtushwa na kifo cha aliyekuwa kiungo wa klabu ya Ligi Daraja ya nchini Italia maarufu kama Serie B ya Livorno aitwae Piermario Morosini. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikuwa akicheza kwa mkpo katika klabu hiyo akitokea klabu ya Ligi kuu ya Udinese alikufa baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati wa mchezo baina klabu hiyo na Pescara uliochezwa jana. Blatter alikaririwa na gazeti moja la michezo nchini Italia kusikitishwa na kifo cha mchezaji huyo na kusema kuwa alikosa neno la kusema baada ya kusikia kifo cha mchezaji huyo zaidi ya kutokwa na machozi. Baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu nchini humo wameonyesha kusikitishwa na kifo hizo na kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia ya mchezaji huyo wakiwemo nyota wa zamani wa Inter Milan, Javier Zanetti na kiungo wa Juventus, Claudio Marchisio. Kufuatia kifo cha Morosini ambaye pia amewahi kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya nchi hiyo, Shirikisho la Soka nchini Italia limesimamisha yote ya ligi za nchi hiyo mpaka hapo baadae.

No comments:

Post a Comment