Wednesday, April 4, 2012

BRAZIL SAYS STADIUMS ON SCHEDULE.

SERIKALI ya Brazil imesema kuwa ujenzi wa viwanja katika miji 12 vitavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia unakwenda vizuri na utakamilika kwa wakati. Zikiwa zimebakia siku 800 kabla ya michuano hiyo serikali ya nchi hiyo imesema zaidi ya nusu ya ujenzi katika viwanja vitano tayari umekamilika huku viwanja vingine vitano vikiwa ujenzi wake umefikia asilimia 30 na viwili vilivyobakia asilimia 20. Viwanja ambavyo ujenzi wake umefikia asilimia 20 ni Uwanja wa Beira-Rio uliopo kusini mwa jiji la Porto Alegre na Arena das Dunas uliopo Kaskazini Mashariki ya Natal, Uwanja wa Castelao Kaskazini Mashariki mwa jiji la Fortaleza umekaribia kumalizika baada ya ujenzi wake kufiki asilimia 60. Katika hatua nyingine Baraza la Seneti ya nchi hiyo limesema kuwa linataka kuzungumzia muswada wa Kombe la Dunia na Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil Sepp Blatter na sio Katibu wake Mkuu Jerome Valcke. Mwezi uliopita Valcke aliingia katika mzozo na serikali ya nchi hiyo baada ya kulalamika kuhusu maandalizi ya taratibu yanayofanywa na nchi hiyo kuelekea kwenye michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment