Thursday, April 5, 2012

BRAZIL: RECIFE SET TO HOST CONFED CUP.

KAMATI ya Maandalizi ya Kombe la Dunia ya nchini Brazil imesema kuwa mji uliopo Kaskazini Mashariki wa Recife utakuwa tayari kusaidia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho pamoja na maandalizi ya taratibu katika mji huo. Rais wa Kamati hiyo Jose Maria Marin alitembelea mji huo jana na kusema kuwa ana imani kuwa ujenzi unaoendelea hivi sasa utakamilika ndani ya muda kwa ajili michuano hiyo ambayo inatarajiwa mwaka kesho. Marin aliutembelea mji huo baada ya kukutana na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wiki iliyopita ambapo shirikisho hilo lilionyesha wasiwasi wake kama mji huo utakuwa tayari ndani ya muda uliopangwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo. FIFA itatoa maamuzi yake June mwaka huu kama Racife itakuwa moja ya miji ambayo itakuwa mwenyeji wa Kombe la Shirikisho au la.

No comments:

Post a Comment