Saturday, March 24, 2012
Tulisa - " We are Young "
HAVE BLESSED SUNDAY EVERYONE!!!!!!!!!!!!
VURUGU ZAISABABISHIA ADHABU GOR MAHIA.
BODI ya Viwanja vya Michezo nchini Kenya (SSMB) imeifungia klabu ya Gor Mahia kutumia Viwanja vya Nyayo na Moi International Sports Centre Kasarani. Hatua hiyo inakuja baada ya vurugu za mwishoni mwa wiki katika mechi yao na wapinzani wao wa jadi, AFC Leopards ambayo ilivunjika baada ya dakika 26 tu. Uamuzi huo umefikiwa kutangazwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Generali Mstaafu Daniel Opande. Pamoja na hayo, uamuzi hao haupokewa vizuri na Gor Mahia ambayo imechukuliwa kama ni wa haraka. Kifungo hicho kinawafanya Gor Mahia wawe na Uwanja mmoja tu wa kutumia, City ambao hauendani na idadi kubwa ya mashabiki wao
Friday, March 23, 2012
WENGER WANT QUALITY NOT QUANTITY.
KOCHA wa Arsenal amewaonya mashabiki wa timu hiyo kuwa wasitegemee mabadiliko makubwa katika klabu yake mwishoni mwa msimu huu kwasababu amepanga kununua wachezaji wenye majina makubwa. Mashabiki klabu hiyo wamekuwa na hasira na kocha huyo kutokana na kushindwa kusajili wachezaji ambao watakata kiu ya timu hiyo kukosa vikombe kwa miaka saba sasa nab ado wamendelea kumhimiza kutafuta wachezaji wazuri msimu ujao. Lakini Wenger ambaye Ijumaa alikataa taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ujerumani Lukas Podolski amefanyia vipimo vya afya katika harakati za kujiunga na klabu hiyo ameamua kusajili wachezaji ambao anaamini kuwa watakuwa na kipaji kulingana fungu atakalokuwa nalo. Akihojiwa Wenger amesema kuwa kwasasa wana idadi ya wachezaji 25 huku wengine wengi wakiwa wancheza kwa mkopo katika klabu zingine na pia wamecheza bila Jack Wilshere na Abou Diaby karibu msimu mzima kutoka majeraha waliyonayo ambapo kama wachezaji hao wakirudi na kikosi kitaimarika zaidi kwani hata sasa wako katika nafasi nzuri bila kuwa na hao wachezaji. Kwasasa kocha huyo anakiwa kuhakikisha timu hiyo inamaliza ikiwa juu ya Tottenham Hotspurs na Chelsea katika nafasi ya tatu mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ili kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya msimu ujao.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
KUONA MORO UNITED, AFRICAN LYON 1,000/-
Viingilio kwenye mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Moro United na African Lyon itakayochezwa kesho (Machi 24 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Ephraim Ndissa na Abdallah Selega wakati mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga. Wote pia wanatoka Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni James Mhagama kutoka mkoani Ruvuma. Pia viingilio hivyo ndivyo vinavyotumika kwa mechi zote za Ligi Kuu ya Vodacom zinazochezwa Uwanja wa Chamazi zisizohusisha timu za Simba na Yanga. VPL itaendelea tena Machi 28 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi.
MMOJA AONGEZWA TWIGA STARS
Kocha Charles Boniface Mkwasa wa Twiga Stars amemuongeza mshambuliaji Rehema Salum wa Shule ya Sekondari Lord Baden ya mkoani Pwani kwenye kikosi hicho kitakachoingia kambini Machi 25 mwaka huu. Rehema aliibuka mfungaji bora kwenye mashindano maalumu ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoshirikisha shule nane za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na kuhitimishwa Machi 8 mwaka huu. Twiga Stars itaingia kambini kwenye kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyoko Ruvu mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Fainali za Wanawake Afrika (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea. Timu hiyo itacheza na Ethiopia kusaka tiketi ya kwenda Equatorial Guinea ikianzia ugenini Addis Ababa kwa mechi itakayochezwa Mei 26 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam. Katika raundi ya kwanza, Twiga Stars iliitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-2. Ilishinda ugenini 2-0 na kuibuka na ushindi mnono nyumbani wa mabao 5-2. Machi 10 mwaka huu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alizindua akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ili ishiriki vyema michuano ya AWC. Wachangiaji wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja ni sh. 500,000. Katika uzinduzi huo, Waziri Dk. Mukangara alichangia sh. milioni moja.
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani kwa kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji na mechi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Machi 31 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA). Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.

Kim Kardashian amwagiwa unga wa ngano kwenye red carpet
Kim Kardashian amwagiwa unga wa ngano akiwa kwenye red carpet siku ya uzinduzi wa parfyum yake huko West Hollywood marekani. Inasemekana mtu aliefanya kitendo hicho, ambae ni mwanamke alirusha unga huo huku akisema "this is for Kris Humphries". Kris Humfphries alikua mume wa Kim ambae walifunga ndoa ambayo ilidumu kwa miezi mitatu tu august 2011-october 2011.
Alipoingia
akiweka pozi la picha
Baada ya kumwagiwa unga
Baada ya kufanya tukio hilo dada aljaribu kukimbia ila alikamatwa na kuachiwa baadae kwa kuwa Kim K hakumfungulia mashtaka. Kim alienda kujisafisha na kurudi kuendelea na shughuli yake kama kawaida.
Hapo ingekua star wa kibongo sasa...angetaka kupigana, kutukanana etc.

Subscribe to:
Posts (Atom)