Tuesday, April 3, 2012
PARK ATABIRI KOMBE LA DUNIA KWENDA ASIA NDANI MUONGO MMOJA.
KIUNGO wa Manchester United Park Ji-Sung ametabiri kuwa nchi moja kutoka bara ya Asia itanyakuwa Kombe la Dunia ndani ya miaka 10 ijayo. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Korea Kusini alinukuliwa na gazeti moja nchini China akisema kwamba timu za bara la Asia bado zina safari ndefu kufikia mafanikio hayo lakini watafikia huko haraka. Park amesema kuwa bado kuna nafasi kubwa kati ya Asia na timu za Ulaya ambazo ndio zinaongoza duniani kwa soka hivyo wana safari ndefu ingawa katika miaka ya karibuni wamekuwa wakionyesha soka safi ambalo wanaweza kulingana na timu za huko. Mpaka sasa kiwango bora kilichoonyeshwa na timu kutoka bara la Asia ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 2002 wakti Korea Kusini ilipokuwa mwenyeji wa michuano hiyo na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali. Michuano mingine ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil ikifuatiwa na itakayofanyika Russia 2018 na ile Qatar 2022.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
TFF YAIPOKA POINTI YANGA
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Aprili 2 mwaka huu) kupitia ripoti mbalimbali za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza umezingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji. Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.” Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezaji amekosa mechi mbili tu. Pia klabu za Coastal Union na Yanga zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1). Kamati ya Ligi pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza. Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum. Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad, Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.
TWIGA STARS YASAIDIWA JEZI ZA MAZOEZI
Kampuni ya Galileo by Travelport Tanzania imetoa msaada wa jezi za mazoezi na maji kwa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) wenye thamani sh. milioni 1.5. Msaada huo umekabidhiwa leo (Aprili 3 mwaka huu) na Meneja Biashara wa Galileo by Travelport Tanzania, Margret Leslie ambaye amesema wameitikia mwito wa kuisadia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali inayoikabili. TFF imeishukuru kampuni hiyo ya uwakala wa tiketi za ndege kwa msaada huo na kuzitaka kampuni, taasisi na watu binafsi kujitokeza kuisaidia Twiga Stars ambayo kwa sasa haina mdhamini, kwani gharama za mashindano ni kubwa.
TFF YAPONGEZA WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo kwa kushinda tuzo ya uandishi bora ya EJAT inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Waandishi hao walioshinda katika kategori ya mpira wa miguu ni Imani Mani wa Daily News (magazeti), Abdallah Majura wa 91.2 Sport FM (redio) na Anuary Mkama wa Mlimani Media (televisheni). TFF inawapongeza waandishi hao kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu, lakini pia ni changamoto kwa waandishi wengine ambao hawakufanikiwa kushinda. Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika ustawi wa mpira wa miguu, kwani katika nchi nyingine vimefichua rushwa katika mpira wa miguu. Ni matarajio yetu kuwa vyombo vya habari nchini navyo vitakuwa mstari wa mbele katika kufichua na kupambana na rushwa katika mpira wa miguu nchini.

MAUMIVU YA BEGA KUMUWEKA NJE SAMATTA.
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa muda zaidi kutokana na maumivu yake ya bega aliyoyapata wiki iliyopita mjini Kitwe Zambia, akiichezea klabu yake Tout Puissant Mazembe dhidi ya Power Dynamos ya huko katika Ligi ya Mabingwa Afrika.Taarifa kwenye tovuti ya TPM imesema leo kwamba, Samatta akiwa Kenya alilazimika kusimama kwa muda kutokana na kuzidiwa kwa maumivu na hiyo inamaanisha hataweza kucheza mechi ya Jumapili dhidi ya Dynamos.
Samatta aliyefunga bao la Mazembe katika sare ya 1-1 ugenini kwenye mechi hiyo ya kwanza, Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa hataweza kucheza mechi ya marudiano Jumapili. TP Mazemebe imepata pigo linguine, mchezaji wake kufuatia kifo cha baba wa mchezaji wao, Francis Kalala ‘Postolo’, Kasongo Ngongo aliyezaliwa mwaka 1946.

VILLA'S PETROV IN POSITIVE MOOD.
NAHODHA wa klabu ya Aston Villa, Stiliyan Petrov yupo katika hali nzuri kiakili kabla ya kuanza kwa matibabu yake ya kansa ya damu mwishoni mwa wiki iliyopita. Mchezaji mwenzake ambaye walicheza wote katika klabu ya Celtic, John Hartson amesema kuwa afya aliyokuwa nayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 raia wa Bulgaria itamsaidia kupambana na ugonjwa huo unaomkabili. Mchezaji huyo anaamini kuwa Petrov atakiruka kiunzi hicho kigumu katika maisha yake kwa kuwa nguvu anazo na anajua kuwa ulimwengu wote wa soka uko nyuma yake katika kipindi hiki kigumu. Hartson ambaye nae alifanikiwa kupambana na ugonjwa wa kansa ya pumbu ambayo kitaalamu inaitwa Testicular mwaka 2009 amesema kuwa aliongea na Petrov Jumapili kabla hajaanza kupata matibabu katika Hospitali moja inayoshughulika na magonjwa hayo iliyopo jijini London na kwamba yuko katika hali nzuri.
SAFA YAZIDAI MIJI WENYEJI WA AFCON RANDI MILIONI 22.
CHAMA cha Soka nchini Afrika Kusini-SAFA kinadai kiasi cha randi milioni 22 kwa kila mji utakaotumika kama mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani. SAFA kinatafuta fedha kwa ajili ya kufidia gharama ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kutumia kiasi cha zaidi ya randi milioni 100 ambapo miji hiyo saba itakayokuwa mwenyeji itatakiwa kulipa kiasi hicho au watanyimwa nafasi hiyo. Suala hili lilijulikana baada ya jiji la Cape Town kutaka kujitoa katika kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji kwasababu hawataki kutumia pesa za walipa kodi wao kwa ajili mpira. Diwani wa jiji la Cape Town Grant Pascoe amesema mji wake huo una nia ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ndio maana wametuma barua ya maombi lakini kwa kiwango ambacho SAFA wanadai hawataweza kukimudu.
BEKI WA ATALANTA AKAMATWA KWA KASHFA YA UPANGAJI MATOKEO.
BEKI wa Atalanta, Andrea Masiello amekamatawa baada ya taarifa kwamba alihusika na upangaji wa matokeo na wachezaji wenzake wanane wa zamani wa Bari na suala lao lipo chini ya uchunguzi. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Italia imesema kuwa upangaji wa matokeo unazorotesha maendeleo ya soka nchini humo na wameahidi kuchukua hatua kwa atakayekutwa na hatia. Tangu kundi la kwanza la watu 16 wakamatwe Juni, mwaka jana, watu wengine 30 wamekamatwa, akiwemo nahodha wa zamani wa Atalanta, Cristiano Doni na nahodha wa zamani wa Lazio, Giuseppe Signori. Mechi tisa za mwisho za Bari msimu uliopita zinachunguzwa, kwa mujibu wa shirikisho, ikiwemo mechi ambayo bao la kujifunga la Masiello liliisaidia Lecce kushinda 2-0 na kuepuka kushuka daraja, baada ya Bari kuwa tayari imeshuka.
UONGOZI WA AL WASL WAMKINGIA KIFUA MARADONA.
KLABU ya Al Wasl ya Dubai imesema kwamba kocha wao, Diego Maradona alifanya jambo la heshima baada ya kuteremika jukwaani kuwavaa mashabiki waliokuwa wanamzomea mpenzi wake na wake za wachezaji wa klabu hiyo. Al Wasl imesema kwenye tovuti ya klabu hiyo leo kwamba hasira za Maradona zilikuwa zinaeleweka na alifanya jambo la heshima mwishoni mwa wiki. Abdullah al-Bishr pia alimuomba radhi gwiji huyo wa Argentina, ambaye alianza kuifundisha timu hiyo mwaka jana. Maradona alipambana na mashabiki wa timu pinzani, Al Shabab ambao waliwazomea wanawake wa wachezaji wa timu yake ambayo katika mchezo huo walifungwa mabao 2-0. Maradona aliwaita mashabiki wa Al Shabab ni waoga.
Subscribe to:
Posts (Atom)